Hali nchini Syria yazidi kuzorota, watu 22 wameuawa
Imechapishwa:
Takriban watu ishirini na wawili wameuawa mjini Hama nchini Syria walipukuwa katika juhudi za kuvamia mji huo kwa kuondoa vizuizi vilivyowekwa na wakazi wa mji huo baada ya maandamano makubwa shirika la kutetea haki za binaadam la nchini humo limethibitisha.
Wakazi wengi wa mjini humo wameyakimbia makazi yao na kuelekea mini Al Salamiya na Damascus huku taarifa zikisema ku
wa vikosi hivyo vinaendelea na operesheni yao ya kutafuta,kuua na kuwakamata raia.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam,Amnesty International limeshutumu mamlaka ya nchini Syria kwa kukiuka haki za binaadam wakati wa maandamano yaliyofanywa na raia kupinga utawala wa rais wa nchi hiyo,Bashar Al Assad.