Wanajeshi husika na ubakaji mashariki mwa DRC wajisalimisha
Kanali wa jeshi nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Nyiragire Kulimushi na wanajeshi wengine takriban 200 wanaoshutumiwa kwa makosa ya ubakaji mashariki ya DRC wamejisalimisha katika jeshi la nchi hiyo. Msemaji wa jeshi la kongo amethibitisha.
Imechapishwa:
Kulimushi,maarufu kwa jina la Kifaru,alijitokeza waziwazi hadharani jana na wanajeshi 116 baada ya kuwa mafichoni na kuwasili katika kituo cha mafunzo cha kijeshi, Luberizi katika jimbo la kivu kusini.
Luteni kanali nchini humo,Sylvain Ekenge amesema hakukuwa na masharti juu ya yaliyowekwa yaliyosababisha kujisalimisha,na kuongeza kuwa Kulimushi alipewa amri ya kujitokeza na kujisalimisha,na hivi sasa yuko chini ya mamlaka huku akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake.