Bei ya mafuta kupungua nchini Marekani na China
Imechapishwa:
Bei ya mafuta imeelezwa kuendelea kushuka kufuatia kutolewa kwa takwimu zisizoridhisha toka kwa nchi za China na Marekani ambao ni watumiaji wakubwa wa nishati hiyo.
Wachambuzi wa masuala ya uchumi wamesema kuwa mpaka kufikia mwezi wa nane mwaka huu, soko la mafuta mjini new york linatarajiwa kushuka kutoka dola 95.o8 kwa pia hadi dola 1.8 kwa pipa.
Wachambuzi hao wamesema kuwa kushuka kwa bei ya mafuta nchini marekani na China kunatokana na takwimu zilizotolewa na nchi ya Marekani zinazoonyesha kuwa kwa mwezi wa sita peke yake ajira zilitengenezwa zilikuwa ni elfu 18 ambacho ni kiwango cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa nchini humo.
Wameongeza kuwa hali hiyo huenda ikachangia kushuka kwa uchumi wa mataifa hayo mawili makubwa ambayo ni wanunuzi wakubwa wa mafuta huku nchi nyingine pamoja na wafanya biashara wakiathirika.