Marekani -Afghanistani

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistani

Tempsreel

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amewasili nchini Afghanistan hii leo kwa ziara ya kushtukiza kukutana na vikosi vinavyofanya kazi na jumuia ya majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi NATO. Alipowasili katika mkoa wa Kapisa, rais Sarkozy alijielekeza moja kwa moja katika kituo cha wanajeshi wa Ufaransa cha Tagab, eneo la mapambano ya hapa na pale baina ya vikosi hivyo na waasi wa Taliban.

Matangazo ya kibiashara

Sarkozy amekuwa na mazungumzo juu ya maendeleo ya jeshi lake na jenerali Emmanuel Moorin kabla ya kuwa na mazungumzo na vikosi vya ufaransa.

Baada ya hayo atarejea mjini Kaboul kuzumza na kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan David Patreas na baadae atakuwa na mazungumzo na rais wa nchi hiyo Hamid Kharzai. Artakutana pia na raia wa Ufaransa waishio mjini Kaboul kwenye ubalozi wa Ufaransa

Mwezi uliopita Sarkozy alitangaza hatuwa ya nchi yake kuvindowa vikosi vya Ufaransa  nchini Afghanistan kabla ya mwisho wa mwaka huu, sambamba na vile vya Marekani,  ukiwa ni mchakato wa kurudisha jukumu la usalama kwa majeshi ya Afghanistan.

Zaidi ya wanajeshi elfu 4 wa Ufaransa walitumwa huko Afghanistani, 64 waliuawa tangu yalipoanza mapambano nchini Afghanistani mwaka 2001, ambapo 12 kati yao waliuawa mwaka huu.