Syria yamshutumu vikali waziri wa nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton
Imechapishwa: Imehaririwa:
Serikali ya Syria imemshutumu vikali waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton kufuatia matamshi yake iliyoyaita ya kichochezi dhidi ya utawala wa Rais Bashar Al Asad.
Kauli hiyo ya serikali ya Syria imekuja saa chache kufuatia matamshi aliyoyatoa Hillary Clinton ya kuuita utawala wa Rais Asad kuwa umepoteza mamlaka nchini humo na hauna nguvu tena kutawala nchi hiyo.
Kauli hiyo inakuja kufuatia waandamanaji wanamuunga mkono rais Asad kuvamia balzoi za Ufaransa na Marekani kushinikiza waondoke nchini humo.
Wizara ya mambo ya nje ya Syria katika taarifa yake imesema kuwa kamwe haitatishwa na vitisho vya Marekani na utawala wa rais Asad ni utawala halali.