Pakistani

Watu 14 wauawa kwa shambulio la bomu nchini Pakistani

l'express

Watu 14 wamekufa na wengine watatu wamejeruhiwa kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa ndani ya saa 24 kaskazini mashariki mwa Pakistan katika jimbo la waziristan.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo ambayo ni muendelezo wa mashambulizi mfululio yaliyoanza kutekelezwa tangu usiku wa jumatatu yameshuhudia yakiua watu 14 na kujeruhi wengine katika mji wa Drey Nashtar kusini mwa jimbo la waziristan.

Shambulio hilo limekuja ikiwa zimepita saa chache baada ya serikali ya Marekani kutangaza kusitisha msaada wa kifedha wa zaidi ya dola milioni 800 kwa majeshi ya pakistan yaliyoko katika mji huo.

Maofisa usalama katika eneo hilo wamewashutumu wapiganaji wa kundi la Al Qaeda na Taliban kwa kuhusika katika mashambulizi hayo.