Kikosi cha wokozi majini nchini Urusi cha faanikiwa kunasua miili ya watoto waliokuwa wamenaswa
Urusi imesema takriban watu 116 wamekufa maji baada ya boti iliyokuwa ikifanya safari zake kupinduka na kuzama katika mto volga baada ya kupigwa na tufani siku ya jumapili.
Imechapishwa:
Kikosi cha wokozi majini nchini urusi kimefanikiwa kunasua miili ya watoto waliokuwa wamenasa katika chumba cha kucheza katika boti hiyo.
Bendera zimepepea nusu mlingoti nchi nzima na kusitishwa kurushwa kwa vipindi vya muziki kwenye televisheni kuonesha ishara ya heshima na maombolezo kwa wale waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Kamati inayochunguza chanzo cha ajali imethibitisha kuwa vifo hivyo vimesababishwa na uzembe wa waongozaji wa chombo hicho na tayari wahusika wanashikiliwa na mamlaka ya nchi hiyo.