Misri-Maandamano

Maelfu waandamana nchini Misri kushinikiza kuangushwa kwa uongozi wa kijeshi

Maelfu ya raia wa Misri wameandamana hapo jana kushinikiza kuangushwa kwa kiongozi wa kijeshi nchini humo kwa kile kinachoelezwa kuto ridhishwa kwao na namna jeshi la nchi hiyo linavyofanyia kazi mabadiliko tangu utawala uliopita ulipoondolewa madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wanadai kuangushwa kwa kiongozi wa baraza la kijeshi Hussein Tantawi aliyekuwa waziri wa ulinzi kipindi cha utawala wa Mubarak.

Waandamanaji wamekuwa wakiweka kambi katika viwanja vya Tahrir,mjini Alexandria tangu maandamano ya nchi nzima yalipoanza siku ya ijumaa kushinikiza kufanyika mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Miezi mitano baada ya kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo,Hosni Mubarak,wanaharakati wanatilia shaka kuwa mapinduzi yanaelekea kushindwa na wanaishutumu baraza tawala la kijeshi kushikilia madaraka hali ambayo inazuia juhudi za kufungua milango ya kidemokrasia nchini Misri.