Yemen-Marekani

Naibu mshauri wa usalama wa Marekani atowa wito wa kufanyika mabadiliko nchini Yemen

Yahoonews

Naibu mshauri wa usalama nchini Marekani, John Brenner ametoa wito kufanyika kwa mabadiliko haraka nchini Yemen, wito uliotolewa katika mazungumzo ya siku mbili yaliyofanyika kati yake na maafisa wa juu wa serikali ya Yemen mjini Sanaa.

Matangazo ya kibiashara

Brenner amesema ni muhimu kwa pande mbili kushiriki katika mchakato wa mabadiliko ya kisiasa ili kuweza kuwapatia raia wa nchi hiyo huduma bora za kijamii,kiuchumi na usalama imara.

Brenner alikutana na waziri mkuu wa nchi hiyo, Abdrabuh Mansur Hadi na waziri wa mambo ya nje Abu Bakar Al Qirbi sambamba na maafisa wa kijeshi,viongozi wa vyama na viongozi wa asasi za kiraia.

Ubalozi wa Marekani nchini Yemen umesema serikali ya Marekani imeahidi kutoa mchango wake kwa ajili ya utekelezaji wa mchakato wa mabadiliko ya kisiasa nchini humo.