Marekani-Syria

Rais Obama asema, Bashar al Asad amepoteza uhalali wa kutawala Syria

Barack Obama  Julay 11 2011.
Barack Obama Julay 11 2011. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Barak Obama amesema kiongozi wa Syria, Bashar al Assad amepoteza uhalali wa kutawala nchi hiyo, kauli iliyokuja bada ya kuvamiwa kwa ubalozi wa Marekani na ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Akiongea na televisheni ya CBS nchini marekani Obama amesema Assad amepoteza fursa nyingi za kufanikisha kufanyika mabadiliko nchini Syria na kuongeza kuwa katika utawala wake kumekuwa kukifanyika vitendo vya ukatili dhidi ya watu wake ,hali ambayo imemfanya kupoteza maana mbele ya watu wake.

Obama ameikemea Syria akisema kuwa serikali yake itafanya kila liwezekanalo kulinda ubalozi wake.

Nae Naibu waziri wa mambo ya nje wa marekani anayeshughulikia maswala ya hali za binaadam,Michael Posner ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa Syria itawekewa vikwazo zaidi ya vile vilivyotiwa saini na Obama mwezi mei.

Vikwazo hivyo vitafanya marekani kuzuia mali zote za Assad zilizo nchini Marekani,na kuzuia mtu mmoja mmoja na kampuni za marekani kuwa na uhusiano na serikali ya Assad.