Rais wa Afghanistani aongoza shughuli za mazishi ya nduguye mjini Kaboul
Imechapishwa: Imehaririwa:
Maelfu ya wananchi wakiongozwa na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai leo wamejitokeza katika mazishi ya Ahmed Wali Karzai mdogo wa rais wa nchi hiyo aliyeuawa siku ya jumanne mjini Kandahar.
Rais Karzai aliwaongoza maelfu ya wananchi hao katika mazishi ya mdogo wake huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika eneo hilo kwa ndege za majeshi ya NATO kwa kushirikiana na vikosi vya serikali wakionekana kupiga doria kwa muda wote wa wa mazishi.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa mapema kabla ya kufanyika kwa mazishi hayo kulisikika milio ya risasi na mabomu ambapo gavana wa jimbo la helmand Gulab Mangal alinusurika kifo katika shambulio lililolenga gari alilokuwa akitumia .