Libya -Benghazi

Waasi wa Libya washtumiwa kujihusisha na uharibifu wa mali na unyanyasaji

Waasi wa Libya wakifurahia kuuteka uwanja wa ndege wa Misrata Mei 11.2011
Waasi wa Libya wakifurahia kuuteka uwanja wa ndege wa Misrata Mei 11.2011 AFP /Ricardo Garcia Vilanova

Waangalizi wa maswala ya haki za binaadam wamevishutumu vikosi vya waasi nchini Libya kuhusika na vitendo vya unyan'ganyi, uharibifu wa mali na unyanyasaji.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo limesema limekuwa likishuhudia baadhi ya vitendo hivi ambavyo vinaripotiwa kufanyika mwezi june halikadhalika mwezi huu wakati waasi walipokuwa wakiwa katika juhudi za kudhibiti eneo la kusini mwa mji wa Tripoli.

Wanaharakati hao wamesema Katika miji minne inayodhibitiwa na waasi kumeonekana kuwa na uharibifu mkubwa uliofanywa na waasi kama kuharibiwa kwa mali,kuchomwa moto kwa makazi,uvamizi kwenye hospitali na maduka,halikadhalika watu kadhaa kupigwa wakishutumiwa kuunga mkono vikosi vya serikali ya Muamar Gaddafi.

Shutma hizo zinatishia kuharibu taswira ya waasi katika jumuia ya kimataifa pia inaelezwa kuwa shutma hizo huenda zitaikanganya jumuia ya majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi,NATO. Waliokuwa wakitoa msaada wa kijeshi kwa waasi ikiwa ni juhudi za kulinda raia wa Libya.