UNHCR kuanza operesheni ya kusafirisha mahema ya ziada katika kambi ya Daadab nchini Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi duniani UNHCR, limetangaza kuanza operesheni maalumu ya kupeleka mahema ya ziada katika kambi za Daadab na kambi mpya ya Ifo nchini Kenya kukabiliana na wimbi la ongezeko la wakimbizi wanaotoka Somalia.

UNHCR 60
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika hilo Adrian Edwards amesema kuwa mpango huo tayari umeanza ambapo wanatarajia kupeleka zaidi ya Tani 100 za mahema siku ya jumapili ambapo pia tani nyingine 600 zitawasili juma lijalo kwenye makambi hayo.

Shirika hilo pia limepongeza uamuzi wa serikali ya kenya ya kuruhusu kupanua kambi hiyo na kufungua mpaka wa nchi yake na Somalia ambapo uamuzi uliotangazwa siku ya alhamisi na waziri mkuu Raila Odinga alipotembelea kambi hizo.