Uturuki-Libya

Uturuki yatowa msaada wa Euro Bilioni 3 kwa waasi

Ahmet Davutoglu na Mustapha Abdeljalil
Ahmet Davutoglu na Mustapha Abdeljalil REUTERS/Esam Al-Fetori

Nchi ya Uturuki imetangaza kutoa zaidi ya euro bilioni 3 kwa waasi wa nchini Libya fedha ambazo zitaelekezwa kwaajili ya kutoa misaada ya kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa nchi hiyo umetangazwa hii leo na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu wakati akihutubia mkutano wa viongozi wa nchi za umoja wa majeshi ya kujihami NATO.

Waziri Davutoglu amesema kuwa nchi yake imeona uko umuhimu wa kuwasaidia waasi wanaopigana na serikali wakati huu ambapo mfungo wa mwezi wa ramadhani unakaribia kwaajili ya kuwasaidia wananchi.

Mkutano huo wa viongozi wa NATO unalenga kujadili hali ya mambo nchini Libya na hatua zaidi ambazo zitachukuliwa dhidi ya serikali ya kanali Muamar Gaddafi ambaye bado amebakia madarakani.