Mashirika ya Umoja wa Mataifa UN yafanikiwa kutoa msaada katika maeneo yanayokaliwa na Al Shabab, Somalia
Kwa mara ya kwanza mashirika ya umoja wa mataifa ya kutoa msaada nchini Somalia yamefanikiwa kufikisha chakula katika maeneo ambayo yanakaliwa na wapiganaji wa kundi la Al Shaabab lenye uhusiano na kundi la Al Qaeda.
Imechapishwa:
Msemaji wa shirika linaloshughulikia watoto duniani UNICEF, Rozzane Chorlton amesema kuwa wapiganaji wa kundi hilo walitoa ushirikiano wa kutosha kwa wafanyakazi wa shirika lake na kufanikiwa kuwahudumia maelfu ya watoto na wazazi ambao walikuwa wanahitaji msaada wa chakula wa haraka.
Juma hili kuliripotiwa kutekwa nyara kwa wafanyakazi wawili wa umoja huo na wapiganaji wa Al Shaabab wakati wakijaribu kuingia katika moja ya miji ambayo inashikiliwa na wapiganaji hao na kutishia mashirika mengine kushindwa kufika katika maeneo zaidi.
Nchi ya Uingereza imetangaza kutoa kiasi cha dola milioni 84 kwaajili ya waathirika wa njaa nchini Somalia.