Jeshi la Israeli laendesha mashambulizi katika Ukanda wa Gaza
Jeshi la Israeli limeendesha mashambulizi ya anga jana usiku mashariki mwa mji wa Khan Yunis. watu wawili wamejeruhiwa wapiganaji wa 2 wa Palestina, moja akiwa katika hali mahtuti. Vimethibitisha vyanzo vya habari hii.
Imechapishwa:
Msemaji wa jeshi la Israel alithibitisha uvamizi huo, akisema kuwa Jeshi la Israeli limefanya shambulio hili ili kuwazuia wapiganaji wa Palestina ambao walikuwa na dhamira ya kuendesha shambulizi la kigaidi.
Kulingana na mashahidi wa Palestina, mbali na mashambulizi ya hayo ya bomu, ndege za Israel zimesambaza vipeperushi vinavyo towa onyo kwa wananchi wakazi wa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kutosogelea eneo la kizuizi kinacho gawa upande wa Gaza na Israeli kwa maili ya mita 300.
Mashambulizi ya roketi dhidi ya Israeli kutoka Gaza na mashambulizi ya Israeli ya kulipiza kisase yanaripotiwa siku zote hizi za nyuma. Kulingana na jeshi la Israeli Jumla ya makombora 22 yaliangushwa katika ardhi ya Israeli tangu mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu
Eneo hilo lililkuwa limepata utulivu baada ya uslama kuyumbishwa mnamo siku za hivi karibuni.
Kijana moja wa Israeli aliuawa kwa roketi akiwa katika basi la shule, hivyo israeli ililipiza kwa kuendesha mlolongo wa mashambulizi yaliosababisha kuuawa kwa uchache watu 19 wafu, ambapo ni idadi kubwa kutokea tangu mwanzo wa opereshini ya umwagaji damu wa Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza mwishoni mwa miaka ya 2008 na mapema 2009.