Uingereza

Mkuu wa kituo cha polisi ya Metropolitani ajiuzulu kufuatia kashfa ya uharamia wa taarifa

Sir Paul Stephenson
Sir Paul Stephenson REUTERS/Suzanne Plunkett

Sakata la uharamia wa taarifa kwa njia ya simu ambalo limeikumba nchi ya Uingereza limeendelea kuchukua sura mpya baada ya mkuu wa polisi katika kituo cha metropolitani kujiuzulu nafasi yake kutokana na kashfa hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Akitangaza uamuzi wake Sir Paul Stephenson amesema kuwa ameamua kufikia hatua hiyo baada ya kuona kuna umuhimu wa kufanya hivyo na kuwajibika kama kiongozi huku akisisitiza kuwa hausiki kwa lolote na kashfa ya gazeti la News of the world wala kampuni ya News Corporation.

Wakati huohuo waziri mkuu wa Uingereza david cameron tayari amewasili mjini Johanesberg Afrika kusini kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kukutana na Rias jackob zuma kwa mazungumzo kabla ya kuelekea nchini Nigeria kwa ziara kama hiyo.
Na aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la news corporation rebekah Brooks ameachiliwa huru kwa dhamana muda mchache uliopita baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini wikiendi hii kwa tuhuma za kuhusika katika kashfa hiyo.