Afrika Kusini

Nelson Mandela rais wa zamani wa Afrika Kusini atimiza miaka 93 ya kuzaliwa

Nelson Mandela
Nelson Mandela REUTERS/Mike Hutchings

Maelfu ya raia wa Afrika Kusini hii leo watasherekea kukumbuka siku ya alipozaliwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo na muasisi wa harakati za uhuru wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela ambaye anatimiza umri wa miaka 93 hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Mzee Nelson Mandela mwenyewe tayari amewasili katika kijiji ambacho alizaliwa kwaajili ya kusherekea siku hii, huku maelfu ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakiandaliwa kuimba nyimbo za kumsifu kiongozi huyo kwa harakati zake nchini humo.

Mandela ambaye anakumbukwa kwa kuwa mstari wa mbele wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo, anakumbukwa kwa ujasiri wake wa kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukifanywa na wakoloni pamoja na kutetea haki za watu wa matabaka ya chini.

Kiongozi huyo anasherekea siku hii wakati ambapo bado anaendelewa kupatiwa matibabu akiwa nyumbani ambapo itakumbukwa mwezi wa kwanza mwaka huu alilazwa hospitalini kutokana na kuugua.