Syria-EU

UE yaiwekea vikwazo Syria, Quatar ikifunga Ubalozi wake nchini Dimuscus

le monde.fr

Shinikizo la kujiuzulu kwa serikali ya Syria limeendelea kuongezeka baada ya nchi ya Qatar kutangaza kufunga ubalozi wake mjini Damascus huku Umoja wa Ulaya ukitangaza kuiwekea vikwazo zaidi nchi ya Syria.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya nchi ya Qatar kufunga ubalozi wake nchini humo imeonekana kuwashangaza wengi kufuatia uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ambapo Qatar alikuwa rafiki wa karibu wa Syria kwa kuiunga mkono serikali ya rais Bashar al-Asad.

Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Heague amesema kuwa kunahitajika kuchukuliwa hatua za haraka zaidi kuongeza shinikizo dhidi ya serikali ya Syria kwa kile alichodai vikosi vya nchi hiyo kuendelea na vitendo vya unyanyasaji wa raia.

Maandamano makubwa yamekuwa yakishuhudiwa siku zorte hizi za nyuma, ambapo vikosi vya polisi vimekuwa vikiwamalizia maisha raia katika opereshieni za kutaka kuzima maadamano. Inaarifiwa kutumiwa kwa zana nzitonzito katika operesheni hizo.