Somalia-Jamii ya kimataifa

Wito wa kutowa misaada ya chakula kwa wananchi wa Somalia

Wakimbizi wa Somalia wakipiga foleni kupata msaada
Wakimbizi wa Somalia wakipiga foleni kupata msaada Reuters

Wito umeendelea kutolewa kwa jumuiya ya kimataifa kutoa misaada zaidi ya chakula kwa nchi ya Somalia kufuatia taifa hilo kukumbwa na janga njaa.

Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa mataifa mbalimbali duniani kuhakikisha wanachangisha kiasi cha dola bilioni 1.6 kwaajili ya kusaidia nchi ya Somalia kupata chakula cha kutosha na mahema ya kuwasaidi watu waliokimbia njaa hiyo.

Wakati huohuo nchi ya Marekani imetangaza kupeleka msaada zaidi nchini Somalia huku ikisema haitajihusisha moja kwa moja na wapiganaji wa Al shabab wanaopigana na serikali.