BRUSSELS-UBELGIJI

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wapitisha msaada wa fedha kwa nchi ya Ugiriki

Waziri mkuu wa Ugiriki, Georgios Papandreou (kushoto) akipongezwa na rais wa Umoja huo, Herman Van Rompuy (katikati) pamoja na Jose Manuel Barroso (kulia).
Waziri mkuu wa Ugiriki, Georgios Papandreou (kushoto) akipongezwa na rais wa Umoja huo, Herman Van Rompuy (katikati) pamoja na Jose Manuel Barroso (kulia). Brussels/Council

Viongozi wa ulaya waliokutana mjini Brussels Ubelgiji hatimaye wamekubaliana kwa kauli moja kuipatia nchi ya Ugiriki msaada mkubwa wapili wa fedha ili kunusuru taifa hilo na hali ngumu ya uchumi unayoikumba.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao ambao walianza kwa kujadili hali ya mambo ilivyo nchini Ugiriki kwa sasa, walikubaliana kutoa msaada wa fedha za zaidi ya dola bilioni 150 ikiwa ni awamu ya pili ya fedha za mkopo ambazo nchi hiyo imepatiwa.

Shirika la Fedha Duniani IMF kupitia kwa mkuu wake wa operesheni barani ulaya limepongeza hatua ambayo imefikiwa na viongozi wa mataifa hayo kwa kuridhia kupitisha msaada huo wa fedha ambao utainusuru nchi ya Ugiriki kuendelea kuwa katika hali ngumu ya kiuchumi.

Kwa mara ya kwanza pia katika mkutano huo, ulijumuisha mashirika binafsi ya taasisi za kifedha ambazo nazo zilikubali kuikopesha nchi ya Ugiriki kiasi cha pesa ambazo zimeidhinishwa na viongozi hao.

Mbali na mashirika binafsi kushiriki katika mkutano huo, pia mabenki ya ulaya nayo yalipewa nafasi ya kutoa mchango wao ambapo awali yalitishia kutotoa fedha kwaajili ya kuisadia nchi ya Ugiriki.

Rais wa umoja wa ulaya,Herman va Rompo amesema hatimaye mpango uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu wa kuokoa nchi zenye mzigo wa madeni umefanikiwa.

Akiongea mara baada ya kupitishwa kwa msaada huo wa fedha, waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou ameunga mkono hatua hiyo na kuwapongeza viongozi wa umoja huo kwa kuona umuhimu wa kuisaidia nchi yake.