MAREKANI

Rais Obama kutumia kura ya turufu kutoa mwongozo wa kukabiliana na deni la kitaifa

Rais wa Marekani Barack Obama huenda akatumia uwezo aliopewa na katiba ya nchi hiyo, kutoa mwongozo wa kukabliana na deni la kitaifa la Dola Trilioni 14 nukta 3, ambalo linahatarisha kudorora kwa uchumi wa taifa hilo.

Rais wa Marekani Barack Obama (kulia) na John Boehner (kushoto) spika wa chama cha Republican
Rais wa Marekani Barack Obama (kulia) na John Boehner (kushoto) spika wa chama cha Republican REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa, muafaka haujafikiwa kati ya wabunge wa Repiblican na Democratic kuhusu mbinu ya kulipa deni hilo kabla ya kukamilika kwa makataa ya mpango huo kuanza kutumika terehe mbili mwezi ujao.

Wabunge wa Repiblican wakiongozwa na Spika, John Boehner wanataka mfumo wa kubana matumiz ya fedha utumiwe,huku rais Obama akipendekza pia mfumo huo, ukiandana na utozwaji ushuru zaidi hasa kwa matajiri nchini humo.

Ikiwa makubaliano yeyote hayatakuwa yamefikiwa kufikia tarehe mbili mwezi ujao, huenda serikali ikalazimika kufunga ofisi kadhaa na hata kusababaisha wafayakazi kukosa mishahara hasa wanajeshi.

Juma hili kumetokea majibizano ya maneno na kutupiana tuhuma kwa kila upande kumshutumu mwenzake kwa kushindwa kusimamia suala hilo na kuhakikisha linapitishwa.

Siku ya Jumanne Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani IMF Christine Lagarde aliwataka wabunge wa nchi hiyo kuweka tofauti zao kando na kukubaliana kuhusu kupitishwa kwa bajeti hiyo ya kubana matumizi na kulipa deni linaloikabili nchi hiyo ili kuinusuru kutumbukia katika mgogoro wa kifedha.