NAIROBI-KENYA

Viongozi wa mashirika ya kutoa msaada nchini Somalia wanakutana mjini Nairobi, Kenya

UN Photo/Stuart Price

Mkutano wa mashirika yanayotoa misaada kuwasaidia maelfu ya watu wanaokumbwa na baa la njaa katika pembe ya Afrika unafanyika leo jijini Nairobi nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Nazo ndege za Umoja wa mataifa zinazobeba chakula kupeleka nchini Somalia, zimecheleweshwa na taratibu za safari za ndege mjini Nairobi, huku maelfu ya watu wakizidi kuathirika kutokana na njaa.

Msemaji wa shirika la mpango wa chakula David Orr amesema kuwa huenda ndege hizo zikaondoka jijini Nairobi hivi leo,baada ya safari yao kuidhinishwa .

Umoja wa mataifa unasema,misaada zaidi inahitajika ili kuokoa watu nchini Somalia, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ametoa wito kwa nchi za Saudi Arabia, Kuwait na Qatar kutuma misaada yao.

Zaidi ya watu Milioni tatu wanakabiliwa na jaa nchini Somalia,Kenya,Ethiopia na Djobouti.