Palestina

Polisi wa Palestina washambulia makaazi ya mkuu zamani wa usalama wa ukanda wa Gaza

Mohamed Dahalan alieshambuliwa nyumbani kwake na polisi ya Palestina
Mohamed Dahalan alieshambuliwa nyumbani kwake na polisi ya Palestina Reflets

Polisi wa nchini Palestina wameshambulia eneo la ukingo wa magharibi yaliko makazi ya hasimu wa rais wa nchi hiyo, Mahmoud Abbas hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limemlenga Mohamed Dahlan aliyekuwa mkuu wa maswala ya usalama katika eneo la ukanda wa Gaza aliyefukuzwa kutoka chama cha Fatah mwezi June baada ya kumkosoa Abbas mara kwa mara.

Msaidizi wa Dahlan amesema polisi wamewakamata walinzi takriban ishirini na watatu na wasaidizi na kukamata silaha 16,kompyuta na magari mawili.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Palestina,Adnan Dameri amesema silaha hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na kuwa hakuna anayeruhusiwa kuajiri walinzi wenye silaha bila ruhusa ya mamlaka.

Dahlan alikuwa akishutumiwa kwa kuwa chanzo cha ushindi wa kundi hasimu la Hamas katika eneo la ukanda a Gaza mwaka 2007 wakati alipokuwa mkuu wa maswala ya usalama katika eneo hilo halikadhalika alikuwa akishutumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Dahlan na Abbas wamekuwa mahasimu tangu dahlan alipokuwa akimkosoa Abbas katika vikao mbalimbali na wanaharakati miezi kadhaa iliyopita.