Somalia

Mkuu wa banki ya maendeleo ya Afrika asema vita vya Somalia ndio sababu ya tatizo la njaa katika pembe ya Afrika

se2009.eu

Mkuu wa Bank ya Maendeleo ya Afrika Donald Kaberuka amesema tatizo la njaa ambalo limeikumba eneo la Pembe ya Afrika lilikuwa linazuilika na limeota mizizi kutokana na kushindwa kudhibiti Vita vya Wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Kaberuka amesema kuwa ni lazima watu wakubali kubeba lawama kwa kile ambacho kinatokea kwa sasa kwani tukio hili si kama majanga mengine ambayo yanatokea kwa kushtukiza ikiwemo Tsunami.

Kiongozi huyo wa Banki ya Maendeleo ya Afrika amesema Somalia ndiyo mhusika wa kwanza kwenye janga hili na ndiyo imechangia hali hii kutokana na machafuko ambayo yanaendelea kushika kasi kwenye taifa hilo.