Syria

Marekani ya sisitiza kauli yake kuhusu Syria

waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani  Hillary Clinton
waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton Reuters

Serikali ya Marekani inaamini kwamba majeshi ya Syria yanahusika na vifo vya raia 2,000, waandamanaji waliouawa wakati askari wa kutuliza ghasia wakipambana nao, katika miji mbalimbali nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, ametoa kauli hiyo muda mfupi uliopita na kuongeza kuwa Rais Bashar Al Assad amepoteza uhalali wa kuwaongoza wananchi wa Syria.

Aidha, kiongozi huyo amesema hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN, na vikwazo vilivyowekwa na jumuiya ya kimataifa dhidi ya serikali ya Assad, ni maamuzi muafaka na wanafanya kila liwezekanalo kumdhibiti rais huyo, mtata.
 Waziri huyo ameutaka Umoja wa Ulaya na nchi za kiarabu kumshinikiza rais Assad kuondoka madarakani.

Serikali ya Marekani imetangaza pia kumrejesha balozi wake Robert Ford nchini Syria Alhamisi ijayo ili kurahisisha mawasiliano. Uamuzi huo unajitokeza wakati nchi zingine tayari zimewarejesha nyumbani wawakilishi wake.

Akiitetea hoja hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa marekani Mark Toner amesema kulikuwepo na umuhimu wa kumrejesha Robert Ford mjini Damascus kuboresha mawasiliano na upinzani na kuonyesha wasiwasi ya Marekani kwa serikali ya Assad.

Wakati hayo yakiarifiwa, maaandamano bado yaendelea katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu was Ramadhani. kulingana na watetezi wa haki za binadamu, watu 4 wameuawa jana alhamisi wakati wa maandamano ya baada ya kufturu.

Duru za raia zaarifu kuwa miili ya watu waliouawa juzi zaidi ya 30, imezikwa katika maeneo ya bustani za umma mjini Hama, mji unaokaliwa na waasi ambao kwa sasa umezingirwa na jeshi la Syria.

Upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Ufransa Alain Juppe amesema kuhusu tangazo la rais Assad la kuruhusu mfumo wa vyama vingi, waziri huyo amesema huu umekuja kama uchokozi, kwani muda umepita na maandamano bado yaendelea.