SYRIA

Rais Bashar al-Asad atetea operesheni ya vikosi vyake katika miji ya Hama na Deir al-Zour

Waandamanji nchini Syria wakimkimbiza kupatiwa huduma mmoja wa majeruhi katika maandamano
Waandamanji nchini Syria wakimkimbiza kupatiwa huduma mmoja wa majeruhi katika maandamano Reuters

Watu kumi wamekufa na wengine zaidi ya hamsini wamejeruhiwa nchini Syria kufuatia polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji wanaoipinga serikali ya rais Bashar al-Assad katika mji wa Deir al-Zour.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa viongozi wa shirika la kuetetea haki za binadamu katika mji huo, Rami Abdel Rahman amesema kuwa polisi walivamia katika mji huo na kuanza kuwafyatulia risasi wananchi waliokuwa wakiandamana kushinikiza kujiuzulu kwa serikali ya rais Asad.

Kituo cha taifa cha televisheni nchini humo kimerusha moja kwa moja hotuba ya rais Asad ambaye ameendelea kuwashutumu wanaharakati nchini humo kwa kuchochea vurugu nchini humo.

Katika hotuba yeke hiyo, rais Asad ameendelea kutetea operesheni ambayo inafanywa na majeshi yake katika miji ya Hama na Deir al-Zour akisema kuwa bila kufanya hivyo wanaharakati na wananchi wataendelea kuvunja sheria za nchi kwa kufanya maandamano haramu.

Wakati polisi wakiendelea na operesheni hizo, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ameendelea kutoa wito kwa serikali ya rais Assad kuamuru vikosi vya nchi yake kuacha kuwashambulia wananchi wasio hatia.