AFGHANISTAN-UINGEREZA

Kituo cha Utamaduni wa Uingereza kilichopo Kabul chashambuliwa kwa mabomu

Watu wa wanane wamepoteza maisha kwenye shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye Ofisi za Kituo cha Utamaduni wa Uingereza zilizopo nchini Afghanistan katika Mji Mkuu Kabul na kuna hofu ya idadi ya vifo ikaongezeka.

Matangazo ya kibiashara

Milipuko mitatu mikubwa imesikika na baadaye milipuko miwili mingine ilisikika na kufuatiwa na watu wenye wenye silaha kuvamia Ofisi hizo hatua ambayo imethibitishwa na Mamlaka za Syria na Uingereza.

Kundi la Wanamgambo wa Taliban limethibitisha kuhusika kwenye kupanga na hatimaye kutekeleza shambulizi hilo wakisema ni sehemu ya kusherehekea maadhimisho ya siku ya uhuru walioupata kutoka Uingereza mwaka 1919.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza amethibitisha saa kadhaa baada ya kutokea milipuko na kukiri eneo kubwa la Ofisi ya Kituo cha Utamaduni wa Uingereza limeharibiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje imesema kwa sasa Ubalozi wa Uingereza unashirikian na Mamlaka nchini Afghanistan kuwasaka wale ambao wamehusika kwenye shambulizi hilo lililotokea mapema asubuhi ya leo Ijumaa.

Kwa upande wake Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Afghanistan Siddiq Siddiqui amekiri watu wanane kuuawa wengi wao wakiwa polisi huku wengine kumi wakijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Siddiqui ameongeza kuwa mmoja wa waliojitoa mhanga amebainika kuwa hai lakini mwenye amekanusha kuhusika kwenye tukio hilo wakati huu ambapo eneo hilo bado halijasafishwa.

Msemaji wa Polisi wa Kabul Hashmat Stanikzai mapema alinukuliwa akisema polisi wawili walipoteza maisha pamoja na vijana wengine wawili ambao walikuwa wanafanya shughuli za usafi katika eneo hilo.

Naye msemaji wa Kundi la Wanamgambo wa Taliban Zabihullah Mujahid amejitamba kutekeleza shambulizi hilo kwa madai kuwa hii ni sehemu ya sherehe za kumbukumbu ya uhuru wa nchi hiyo.

Nchi ya Afghanistan imeendelea kushuhudia mashambulizi yakiendelea kushika kasi wakati huu ambapo Rais Hamid Karzai akitaka Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO kuondoka nchini humo na kuacha jukumu la ulinzi kwa serikali.