SYRIA-MAREKANI

Wanaharakati nchini Syria waandaa maandamano kuunga mkono Rais Bashar Al Assad aondoke madarakani

Smoke rises in the city of Latakia August 14, 2011.
Smoke rises in the city of Latakia August 14, 2011. Reuters路透社

Wanaharakati nchini Syria wameitisha maandamano makubwa baada ya kufanyika kwa sarat Ijumaa baadaye hii leo wakiunga mkono kauli ya Rais wa Marekani Barack Obama kumtaka Rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya ya wanaharakati ni muendelezo wa shikizo la upinzani ambao umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Utawala wa Rais Assad uondoke madarakani kutokana na kushindwa kutelekeza demokrasia.

Wanaharakati na wananchi wanajiandaa kwa maandamano hayo wakati ambapo kumekuwa na operesheni za kuwadhibiti wananchi katika miji mbalimbali na tayari Rais Assad amemhakikishia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon kusitisha zoezi hilo.

Saa kadhaa baada ya Rais Assad kumwambia Katibu Mkuu wa UN kuwa atasitisha operesheni ya kijeshi ndipo Rais Obama kupitia ofisa wake akatangaza hatua kumtaka kiongoiz huyo aondoke madarakani na kungwama mkono na washirika wake Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Kama hiyo haitoshi Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akatangaza vikwazo vipya dhidi ya serikali ya Syria ikiwemo kuzuia mali na fedha za nchi hiyo pamoja na kukataza kufanya biashara ya mafuta na nchi hiyo.

Hatua hiyo imeungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN ambalo liliketi hapo jana na kumtaka Rais Assad kuachana na utaratibu wake wa kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa UN Navy Pillay ni miongoni mwa wale ambao waliopata nafasi ya kuzungumza na yeye akaweka bayana hali ya kibinadamu imezidi kuwa mbaya.

Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa UN Navy Pillay

Pillay akachukua nafasi hiyo kutoa ripoti ya kuthibitisha uwepo wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Utawala wa Syria dhidi waandamanaji wanaopinga serikali iliyopo madarakani.

Kufuatia kutolea kwa madai hayo na Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ndipo Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa UN Baashar Jaffar akachukua nafasi hiyo kuyashutumu mataifa ya Magharibi.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa UN Baashar Jaffar

Jaffar ameweka bayana kuwa Mataifa ya Magharibi yamekuwa vinara wa kuingilia masuala ya Syria na kuchangia hata kuharibu uhusiano wa Kidiplomasia sambamba na kwenda kinyume na Haki za Binadamu.

Nchi ya Syria imejikuta kwenye wakati mgumu kutokana na waandamanaji kutaka uwepo wa demokrasia kwenye nchi hiyo wakidai serikali imekuwa ikiendesha vitu vyake kimabavu.

Tangu kuanza kwa kwa maandamano ya wananchi kushinikiza mabadiliko ya utawala nchini Syria zaidi ya watu elfu moja na mia nane wameuawa huku wengine zaidi ya elfu kumi wakiwa wanashikiliwa na polisi.