LIBYA-TRIPOLI

Waasi wa Libya waanza kuukaribia mji wa Tripoli

Waasi wa Libya wakishangilia baada ya kutwaa miji kadhaa nchini Humo
Waasi wa Libya wakishangilia baada ya kutwaa miji kadhaa nchini Humo REUTERS/Bob Strong

Kiongozi wa Libya kanali Moamar Gaddafi amewataka wafuasi wake kuandamana hii leo mjini Tripoli kupinga uasi unaofanyika nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ombi hilo limekuja wakati huu ambapo vikosi vya waasi vikidai kuukaribia mji mkuu, Tripoli na kujinasib kuwa utawala wa miaka 42 wa Gaddafi uko ukingoni.

Gaddafi amewataka raia kuandamana kwa wingi kukomesha vitendo hivyo na kurudisha miji inayodhibitiwa na waasi katika himaya yake.

Gaddafi amemshutumu rais wa ufaransa,Nikolas Sarkozy ambaye nchi yake inasaidia kufanikisha mashambulizi ya anga dhidi ya vifaa vya jeshi lake,na kuwafunza waasi wa nchi hiyo kama washirika wake ili kuiba utajiri wa mafuta wa nchini Libya.

Katika hatua nyingine, milio mikubwa ya mabomu imesikika mjini Tripoli mapema hii leo wakati wa mapambano kati ya vikosi vya gadafi na majeshi ya waasi ambayo wanaelezwa wameanza mashambulizi mjini Tripoli