Ufaransa-Marekani

Dominique Strauss Kahn achiwa huru

DSK
DSK REUTERS/Eduardo Munoz

Jaji ambaye alikuwa anasikiliza kesi ya tuhuma za ubakaji iliyokuwa inamkabili Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Fedha Duniani IMF Dominique Strauss-Kahn ametupilia mbali mashtaka hayo na hivyo kumuacha huru kigogo huyo.

Matangazo ya kibiashara

 

Jaji Michael Obus alilazimika kuitupilia mbali kesi hiyo baada ya Waendesha Mashtaka kuwasilisha pendekezo la kufutwa kwa mashtaka hayo wakiamini hayana ukweli wowote na yalikuwa na lengo la kumchafua tu.

BENJAMIN BREFMAN 24

Baada ya Jaji Obus kutoa uamuzi huo ndiyo Mwanasheria wa Strauss-Kahn, Benjamin Brafman akachukua nafasi hii kuzungumza na waandishi wa habari ambapo akasema umma ulikosema kutokana na kuchukua hatua ya kuhukumu.

 

Kenneth Thomson 24

Naye Mwanasheria wa Nafissatou Diallo, Kenneth Thompson ametoa malalamiko kwa Mahakama kutupilia mbali ombi lake la kuletwa kwa Mwendesha Mashtaka mwingine ambaye angesimamia kesi hiyo.

 

Strauss-Kahn mwenyewe baada ya kufutiwa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili amemshuru mkewe pamoja na familia yake kwa kuwa naye pamoja kwenye kipindi kigumu cha kukabiliwa na tuhuma.