UFARANSA-MAREKANI

Dominique Strauss-Kahn arejea Ufaransa kwa mara ya kwanza baada ya mashtaka yake kutupwa huko Marekani

照片来源:路透社REUTERS/Kena Betancur

Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Fedha Duniani IMF Dominique Strauss-Kahn amerejea kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa tangu akumbane na tuhuma za kutaka kumbaka mhudumu wa hotel huko New York nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Strauss-Kahn amereja nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya mashtaka ya ubakaji yaliyokuwa yanamkabili dhidi ya Nafissatou Diallo kutupwa na Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo kufuatia waendesha mashtaka kuona hakuna ushahidi wa kutosha.

Strauss-Kahn amewasili Jijini Paris akiwa ameambatana na mkewe Anne Siclair na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle wakitoka New York kwa kutumia ndege ya Shirika la Ufaransa na kisha kuondoka eneo hilo kwa kutumia gari aina ya Peugeot nyeusi.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa IMF alikuwa amezungukwa na polisi huku mwenyewe akionekana kutabasamu kwa muda wote licha ya kushindwa kwake kutoa kauli yoyote kwa waandishi wa habari waliokuwa wanamsubiri kwa hamu.

Strauss-Kahn ambaye alikuwa amevalia suti yake nyeusi na shati jeupe alipanda ndege siku ya jumamosi jioni akitokea New Yoek na hii ikiwa ni karibu majuma mawili tangu kufutwa kwa mashtaka ambayo yalielekezwa kwake.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa IMF mwenye umri wa miaka 62 alikamatwa mnamo mwezi May katika Uwanja wa Ndege wa JFK Jiji New York akituhumiwa kufanya hsmabulizi la kumbaka mhudumu wa hoteli.

Waziri huyo wa zamani wa Fedha na Mchumi aliyebobea kutoka Chama cha Upinzani cha Kisoshalisti alikuwa anatajwa kuwa mpinzani sahihi kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu ujao nchini Ufaransa dhidi ya Rais Nicolas Sarkozy.

Wadadaisi wa mambo wanahisi kashfa hiyo huenda ikawa umeweka dosari katika mchakato wake wa kutaka kuwania urais kwenye uchaguzi ambao utafanyika mwakani mwezi April na May.

Kwa mara ya kwanza Strauss-Kahn alikumbana na tuhuma za
kubaka mnamo mwake 2003 nchini Ufaransa ambapo mwandishi Tristane Banon alisema alitaka kubakwa kutokana na mwanachama huyo wa Chama cha Kisoshalisti kumvuta akiwa ghorofani.