ISRAEL

Maelfu waandamana nchini Israel kupinga kupanda kwa gharama za maisha

Maelfu ya waandamanji waliojitokeza nchini Israel kupinga kupanda kwa gharama za maisha
Maelfu ya waandamanji waliojitokeza nchini Israel kupinga kupanda kwa gharama za maisha REUTERS/Nir Elias

Maelfu ya wananchi wa Israel wamejitokeza kwa wingi katika maandamano yaliyofanyika jana jioni kupinga kupanda kwa gharama za maisha na kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Waandaaaji wa maandamano hayo wameyaita ni ya muda wa kusema ukweli na kwamba wananchi wa taifa hilo wanahitaji kuna mabadiliko katika sera za uchumi na demokrasia.

Maandamano hayo ambayo yametajwa kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo yanaendelea kuongeza shinikizo zaidi kwa waziri mkuu Netanyahu kufanya mabadiliko katika sera yake ya uchumi pamoja na kuongeza ajira nchini humo.

Katika maandamano hayo vijana ndio wameonekana kujitokeza kwa wingi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kukashifu utawala wa nchi hiyo kwa kushindwa kuwaletea mabadiliko wananchi wake huku nchi ikiendelea kukumbwa na mtikisiko wa kiuchumi.

Wakati maandamano hayo yakifanyika katibu mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki Moon amezitaka nchi za Israel na Uturuki kufika katika muafaka kufuatia ripoti ya umoja huo iliyotolewa na kuonyesha makomandoo wa Israel walitumia nguvu kuvamia meli ya flotilla na kuwaua wanaharakati saba raia wa Uturuki.