Pata taarifa kuu
Misri-Mahakama

kiongozi wa kijeshi wa Misri kusikilizwa na mahakama ya kesi ya rais wa zamani Hosni Mubarak

Mohamed Husein Tantawi
Mohamed Husein Tantawi ©Reuters
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
Dakika 1

Majaji wa mahakama inayosikiliza kesi ya rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak wameagiza kuitwa mahakamani kutoa ushahidi kiongozi wa baraza la kijeshi linaloongoza nchi hiyo Mohamad Tantawi aliyekuwa waziri wa ulinzi wakati wa utawala wa Mubarak.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo pia imeagiza kuitwa mahakamani hapo kwa mkuu wa majeshi wa sasa pamoja na aliyekuwa makamu wa rais na mkuu wa usalama wa taifa wakati wa utawala wa Mubarak, Omar Suleiman.

Mubarak anakabiliwa na tuhuma za kuagiza polisi kuwaua wananchi waliokuwa wakiandamana kuupinga utawala wake.

Kesi ya kiongozi huyo imeahirishwa mpaka siku ya Jumapili itakaposikilizwa tena na kushuhudia viongozi hao wakitoa ushahidi wao ambao utaweka wazi endapo bwana Mubarak aliagiza kufanyika kwa mauaji hayo.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.