Japan-Uchumi

Uchumi wa Japan waporomoka kwa asilimia 2.1

le jjd

Uchumi wa Japan umeshuka kwa asilimia 2 nukta 1 katika robo ya pili ya mwaka huu,ikilinganishwa na asilimia 1 nukta 3 katika msimu uliopita hali ambayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kushuka kwa uzalishaji bidhaa za viwandani.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu zilizotolewa hii leo na serikali ya Japan zinaonyesha kuwa uwekezaji katika viwanda nchini humo umeshuka kwa asilimia 0 nukta 9 katika kipindi cha miezi mitatu ikilinganishwa na asilimia 0 nukta 2 ambayo ilitolewa hapo awali.

Hali ya uchumi nchini Japan imekuwa tete katika siku za hivi karibuni kufuatia athari zilizotokana na tetemeko la ardhi la Tsunami lililotokea mapema mwaka huu na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu,pamoja na mitambo ya Nuclear ya Fukushima.