Bahraini-EU

Umoja wa Ulaya waitaka serikali ya Baharaini kuwaacha huru kwa dhamana ma dactari wa kishia

Maandamano ya wanaharakati nchini Bahraini
Maandamano ya wanaharakati nchini Bahraini REUTERS/Hamad I Mohammed

Mkuu wa sera za kigeni ndani ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton ametaka kuachwa huru kwa dhamana kwa madaktari, wafuasi wa madhehebu ya kishia waliokuwa wakishikiliwa wakati wa maandamano dhidi ya serikali ya nchi hiyo.  

Matangazo ya kibiashara

Ashton pia ameitaka mamlaka ya Bahrain kutumia mahakama za raia kuendesha kesi za raia kwa kuzingatia haki, uwazi katika kusikiliza kesi hiyo kama ilivyoahidiwa na mfalme Hamad wa nchi hiyo, mwezi uliopita.

Baadhi ya madaktari walioachwa huru waliongoza mgomo wa kutokula kwa zaidi ya wiki moja kupinga kushikiliwa kwao, huku jopo maalum la wataalam likisema kuwa zaidi ya waandamanaji 100 wanaoshikiliwa walikuwa katika mgomo wa kutokula huku wengine 17 wakifikishwa hospitali baada ya kudhoofu kutokana na mgomo huo.

Mamlaka ya Bahrain aliwashtaki madaktari 24 na wauguzi 23 kutoka hospitali moja kwa shutma za kutaka kuuangusha utawala wa Bahrain. Hivi sasa wameachwa huru wakisubiri uamuzi wa mahakama.