Uturuki-Palestine

Uturuki kupeleka meli za misaada katika ukanda wa Gaza zikisindikzwa na manuari za kijeshi

RTBF

Vikosi vya wanamaji wa uturuki vitapeleka meli za misaada katika eneo la ukanda wa Gaza huku waziri mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan akisema kuwa meli hizo hazitavamiwa tena.

Matangazo ya kibiashara

Meli hizo zitashindikizwa na manuari za kijeshi Hali hii imepelekea Israeli kuonyesha wasiwasi wake kuhusu hatua hii ya Uturuki. Uturuki imeapa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama katika eneo la mashariki mwa mediterania wakati wanaposafirisha misaada kuelekea Gaza.

Mwezi Mei mwaka 2010 makomandoo wa Israel waliizingira meli ya Mavi Marmara iliyokuwa ikishutumiwa kuvuka mpaka wa kijeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza na kusababisha waturuki tisa kupoteza maisha hali iliyofanya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo kutetereka.

Wiki iliyopita uturuki ilimfukuza balozi wa Israel nchini humo na kuvunja makubaliano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili.