Pata taarifa kuu
Libya-Tripoli

Mkuu wa baraza la waasi wa Libya awasili jijini Tripoli

Mkuu wa baraza la mpito, Moustapha Abdeljalil, katika mkutano na vyombo vya habari jijini Benghazi, Julay 30, 2011.
Mkuu wa baraza la mpito, Moustapha Abdeljalil, katika mkutano na vyombo vya habari jijini Benghazi, Julay 30, 2011. REUTERS/Esam Al-Fetori
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
Dakika 2

Usalama uliimarishwa jana septemba 10, kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli wakati alipowasili kiongozi wa baraza la taifa nvhinbi Libya Moustapha Abdeljalil. Alipowasili kwenye uwanja huo mara ya kwanza baada ya miezi 7 ya mapigano, Abdeljalil amethibitisha jukumu lake kama kiongozi wa nchi kwa ajili ya ujezi wa taifa la Libya.

Matangazo ya kibiashara

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege Mustafa Abdeljalil alilakiwa na wafuasi wengi wakiwemo wanamapinduzi walijihisi fahari ya kumlinda huku kila moja akitamani kumgusa au kuwa na mawasiliano,ya jicho kwa kiongozi wao.

Moustapha Abdeljalil hatimaye ametua Tripoli baada ya kusitasita kwa muda mrefu. Ujio wake katika mji mkuu sanjari na mwisho wa muda wa siku 10 uliotolewa kwa wafuasi wa Kanali Gaddafi kujisalimisha. Kiongozi huyo alisema "Libya itakuwa huru wakati miji ya Sirte na Bani Walid Sabha itachukuliwa," alisema.

Taarifa za kuondoka kwake jiji Benghazi, zilitangazwa katika dakika ya mwisho kwa sababu za kiusalama, pia ni ishara ya nguvu kutumwa moja kwa moja kwa Gaddafi, kukabiliana na matamshi yake yaliochapishwa hivi karibuni juu ya kuongoza. Kukamatwa kwa Gaddafi kumepewa kipaombele cha pili kwa kiongozi wa CNT.

Katika vyumba vya mapokezi ya uwanja wa ndege, mkuu wa bodi ya mpito alikutana na wazee wa busara wa Tripoli, ikiwa ni pamoja na waadhini na Mashekh, ambao amewapongeza na kuwafahamisha kwamba anawategemea katika ujenzi wa Libya.

Licha ya kwamba ujiowake jijini Tripoli ni kama bado ni ishara tu, kwani kuna mambo mengi kisiasa ambayo atakabiliana nayo. Hata hivyo, kuwasili kwa Abdeljalil Tripoli kunaashiria mwisho wa utawala wa Gaddafi.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.