Marekani

Shereha za kumbukukumbu ya septemba 11 zafanyika nchini Marekani

Kisiwa cha Manhattan, septemba 10, 2011.
Kisiwa cha Manhattan, septemba 10, 2011. REUTERS/Gary Hershorn

Sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya septemba 11 zilianza tangu jana septemba 10  jijini New York katika kanisa la mtakatifu Patrick ambapo ilisomwa ibada ya misa ya kuomboleza tukio la Septemba 11 mwaka 2001, wakati watekaji nyara waliteka ndege 4 za habiria na kuzidungua. wakati huo watu kadhaa walipoteza. Ibada hiyo ilikuwa hasa kwa kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo wakijaribu kuendesha shughuli za uokozi.

Matangazo ya kibiashara

Waendesha shughuli za uokozi walifika kwa wakati katika kanisa la mtakatifu Patrick kudiriki ibada ya misa ya kuomboleza vifo vya waokozi 343 waliopoteza maisha yao wakati wa tukio hilo. Kutokana na uwingi wa watu kanisani hapo wengine walilazimika kufuata ibada hiyo wakiwa nje ya kanisa, huku kukiwa na huzuni na hisia kubwa kwa wanafamilia.

Misa hiyo ilipitishwa kwenye vipaza sauti ili waliokuwa nje ya ukumbi na lmbali kidogo waweze kusikia. Waokozi kutoka kona zote za ulimwengu walimiminika kanisani hapo kuhudhuria shughuli hiyo ya kuomboleza. Waombolezaji hao kutoka sehemu mbalimbali katika ulmwengu huu walitaka kuonyesha uungwaji wao mkono kwa wenzao wa Marekani kama vile Christian Bragard alietoka Ufaransa”Ni wajibu wa kumkumbuka kwa waokozi wote wa Ufaransa. Tangu Septemba 11, waokozi katika dunia wamekuwa familia moja kubwa. Na baada ya kukutana, na mahali popote kama hivi ni moyo unasema."

"Mfaransa huyo ameendelea kusema kuwa Kwa miaka mingi, inaendelea waokozi wa Marekani hawataki kuchukuliwa kama mashujaa. Kwani wao wanachukulia kwamba walitekeleza majukumu yao. Lakani sasa, miaka kumi baadaye, wanashangazwa na jinsi tunavyo wajali. Kila wakati tunapokutana inakuwa shangwe kubwa sana, na mara zote tunapolkewa vizuri."

Upande wake rais wa Marekani Barack Obama amejielekeza jijini New York Jumapili hii kwa sherehe za kumbukumbu ya septemba 11, sherehe hizo zitafanyika katika maeneo yote yalipotokea mashambulizi.
Rais Obama ameanza siku yake New York akisongwa na kazi nyingi, kwanza katika eneo la Ground Zero. Katika kuanza sherehe atasoma ujumbe na baadae atazindua mbele ya familia za wahanga, mnara wa Kumbukumbu ya Septemba 11.

Baada ya hapo, usimamizi wa Shanksville, Pennsylvania ambapo ndege ya nne iliotekwa nyara ilipoangukia siku hiyo. Na kisha jioni rais Obama atarejea jijini Washington kuhudhuria sherehe kwa ajili ya waathirika wa mashambulizi ya Pentagone, itakuwa Virginia. Na mwishowe Barack Obama atahudhuria tamasha katika Kituo cha Kennedy, kwa kumaliza shughuli za kumkumbuka