Libya

Wanawake wa Libya wahusishwe katika kazi na nyadhifa za juu nchini Libya

laprimera

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Libya kuwahusisha wanawake katika kazi na nyadhifa za juu na kulipa uzito wa kipekee swala la usawa wa jinsia katika katiba yao mpya.  

Matangazo ya kibiashara

Aliyekuwa Rais wa chile na Mkuu wa kitengo cha wanawake ndani ya Umoja wa Mataifa, Michelle Bachellet amemlalamikia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu Libya na nafasi ya wanawake katika maswala ya utawala.

Matumaini ya wanawake katika serikali mpya ya Libya hivi sasa yanategemea nguvu ya mkuu wa kamati ya ushauri ya maswala ya kisheria ambaye pia anawakilisha wanawake.

Akizungumza baada ya mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, mshauri maalum wa Ban Ki Moon, Ian Martin amesema kuwa amegundua kuwa kumekuwa na upungufu wa wanawake katika serikali hiyo inayotawaliwa na wanaume alipotembelea mji wa Benghazi wiki iliyopita.