Uturuki-Misri

Waziri mkuu wa Uturuki azuri Misri

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan REUTERS/Umit Bektas

Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amekutana na mawazirir wa nchi za kigeni kutoka matifa ya kiarabu huko Cairo Misri, na anasema ni sharti Umoja wa Mataifa utambue Palestina kama taifa huru na la kujitengemea.

Matangazo ya kibiashara

Palestina inajiandaa kuwasilisha ombi kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 30 mwezi huu wa tisa, ilikutambua rasmi kimataifa, licha ya pingamizi kutoka kwa Marekani, ambayo inasema itatumia kura yake ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa Matifa kupinga hatua hiyo na Isreal kudai kuwa hatua hiyo ni juhudi za kusambaratisha mazungmuzo ya amani.

Kutokana na kuuimarisha umaarufu wake miongoni mwa nchi za Kiarabu, hasa kwa kuchukua msimamo mkali dhidi ya Israel, Waziri Mkuu Erdogan anatarajiwa kusikilizwa kwa makini atakapowahutubia wajumbe kwenye mkutano wa nchi za Kiarabu unaofanyika mjini Cairo.

Erdogan pia atakutana na wawalkilishi wa Baraza la Kijeshi la Misri ambalo sasa linaiongoza Misri kuelekea katika utawala wa kiraia.

"Erdogan atahutubia kwenye chuo kikuu cha mjini Cairo na pia atakutana na wawakilishi wa baraza la kijeshi la Misri pamoja na wa jumuiya mbalimbali zilizoshiriki katika harakati za mapinduzi.

Waziri Mkuu huyo wa Uturuki pia anatarajiwa kuwahutubia wajumbe wanaohudhuria mkutano wa Umoja wa Nchi za Kiarabu mjini Cairo. Wajumbe kwenye mkutano huo walikubaliana hapo jana juu ya kukusanya nguvu ili kuwaunga mkono Wapalestina wanaokusudia kuwasilisha maombi kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ili Palestina iweze kutangaza dola yake huru.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Nchi za Kiarabu walikubaliana juu ya msimamo huo kwenye kikao chao kilichohudhuriwa pia na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas.