Dunia-IMF

Mkuu wa IMF asema hatuwa za kuzuia matumizi makubwa ya fedha, ndicho kitachoimarisha uchumi wa dunia

Reuters/Shannon Stapleton

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde amesema kuwa uchumi wa dunia utaendelea kuimarika endapo mataifa ya ulaya yatachukua hatua zaidi kudhibiti matumizi makubwa ya serikali zao. Kiongozi huyo pia amepongeza hatua ambazo zimechukuliwa na benki kuu za ulaya, Amerika na Asua kuongeza mitaji katika mabenki yao ili kukabilina na mtikisiko wa kiuchumi, hatua aliyoitja kuwa itachangia sana kukabilina na tatizo hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Ni sauti yake Christine Lagarde mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF.

wakati hayo yakiarifiwa Shirika hilo  la fedha duniani IMF limesema litaipatia mkopo Cote D'Ivoire wenye thamani ya zaidi ya dola za marekani milioni 600 kwaajili ya kuisaidia nchi hiyo kukuza uchumi wake kufuatiua wake kusuasua baada ya vurugu za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Katika ripoti yake kuhusu nchi hiyo IMF imesema kuwa mkopo huo utakuwa ukitolewa kwa awamu ndani ya kipindi cha miaka mitatu na kuongeza kuwa hatua ya kuidhinisha mkopo huo inasubiri maamuzi ya bodi ya shirika hilo inayokutana juma lijalo.

Katika hatua nyingine benki ya dunia imesema kuwa ni lazima nchi hiyo ifanye chaguzi zilizo huru na haki kama inataka kujihakikishia uungwaji mkono toka jumuiya ya kimataifa katika upatiwaji mikopo.