Libya-UN

Bendera mpya ya Libya yapepea kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Homepuzz

Bendera mpya yenye rangi nyekundu, nyeusi na kijani ya nchini Libya leo hii imemepepea sambamba na bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. sherehe rasmi za kupeperusha bendera ya libya mpya zimefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York Marekani wakishiriki viongozi mbalibali wa ulimwengu huu.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe za kupandisha bendera hiyo katika jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa zimefanyika kwa kuimbwa kwa wimbo wa taifa wa Libya.

Balozi wa Libya ndani ya Umoja wa Mataifa Ibrahim Aldredi amesema ni furaha mno kuiona bendera ya Libya ikiwa na rangi tatu zenye kuashiria mengi kwa walibya, na kuongeza kuwa anatazamia kuona libya huru inayoheshimu haki za binaadam na usawa miongoni mwa Raia.

wakati hayo yakijiri, Kanali Muamar Gaddafi amesema kuwa baraza la Libya lisifikiri kuwa utawala wake umeangushwa, kwani utawala wake unaungwa mkono na mamilioni ya raia wa Libya

Ishara hiyo ya bendera inaashiria kuwa Umoja wa Mataifa umekubali kulitambua baraza la mpito la libya. Halikadhalika kauli hiyo ya Gaddafi inaonesha kuwa anataka kuonesha kuwa bado ana nguvu