Palestina-UN

Mahmoud Abbas asema hawezi kuwa kigeugeu

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon kwenye makao makuu ya UN Septemba 19. 2011.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon kwenye makao makuu ya UN Septemba 19. 2011.

Mkuu wa mamlaka ya wa Palestina Mahamud Abbas akiwa jijini New York Marekani amesema kwamba hawezi kuwa kigeugeu, anataka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lizungumze lolote kuhusu ombi lake la kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Kiongozi huyo amemthibitishia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwamba atawasilisha ombi hilo siku ya Ijumaa Septemba 23 licha ya juhudi kutoka pande mbalimbali kumtaka asifanye hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Mahmoud Abbas amesema tangu achukuwe uamuzi wa kwenda kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka Palestina kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa, amesema amekuwa katika hali ngumu, kwani amekuwa akipokea ombo kutoka pande tofauti kumtaka aachane na mpango huo.

 Tony Blair, mwakilishi wa Muungano wa (EU, Marekani, Russia na Umoja wa Mataifa) amesema kwamba juhudi zake hazikufua dafu. Waziri wa Ufaransa wa mambo ya kigeni Alain Juppe alionya dhidi ya "mlipuko wa vurugu" huko Gaza. Marekani yao inataka kusikia tu kwamba mazungumzo ya ana kwa ana yanafanyika. Juhudi za Umoja wa Ulaya EU zilizo wakilishwa na Catherine Ashtonzimeshindwa kuleta muafaka

Mahmoud Abbas Alithibitisha kwa Ban Ki-moon kwamba siku ya Ijumaa, Septemba 23 ndio atawakilisha ombi lake rasmi kwa ajili ya kutawazwa Palestina katika Umoja wa Mataifa.

Kutokana na swala hili nyeti , Baraza la Usalama pengine likajaribu kuchelewesha hatuwa za kujadilki ombi hili la Palestina kuhakikisha muafaka unapatikana kabla ya hatuwa ya kupiga kura.

Upande wake Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipendekeza tangu jana Jumatatu kukutana na Mahmoud Abbas, wakati mazungumzo ya moja kwa moja yalikwama miezi ya nyuma. Rais wa ufaransa Nicolas Sarkozy anatajia kukutana na Mahmoud Abbas Jumanne Septemba 20 mjini New York.