Palestina

Mamia ya wananchi wa Palestina waandamana kuwataka viongozi wa dunia kuunga mkono ombi la Palestina

Maandamano ya wananchi wa Palestina wa miji ya Ramallah, Bethlehem
Maandamano ya wananchi wa Palestina wa miji ya Ramallah, Bethlehem REUTERS/Mohamad Torokman

Maelfu ya Wapelestina wameadamana katika miji ya Ramallah, Bethlehem na Hebron huku shule zikifunga na pamoja na ofisi za mamlaka ya Paletsina kushinikiza baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukubali ombi la rais wa Palestina kutaka mamlaka hiyo kutambuliwa kama taifa linalojitegemea na kupata nafasi katika Umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Barrack Obama, anakutakana na waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu na kiongiozi wa Palestina Mahmud Abass huko New York, katika juhudu za kumshawishi rais Abbas kubadilisha wazo lake la kuwaslisha ombi hilo siku ya Ijumaa.

Jambo ambalo mapema Mahmoud Abbas alitangaza kutoweza kamwe kuwa kugeugeu kwa kubadili kauli yake, na kusisitiza kwamba ombi hilo lazima aliwasilishe siku ya Ijumaa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa licha ya vitisho na vitimbi ambavyo amekuwa akivipokea kutoka sehemu mbalimbali.

Marekani inatumia mbinu zake zote kuhakikisha Mahmoud Abbas anabadili msimamo wake na kuketi katika meza ya mazungumzo na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyau

Marekani imeweka wazi kuwa itatumia kura yake ya turufu kama mwanachama wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kupinga ombi hilo,huku Isreal iukisema kuwa amani kati yake na Palestina haiwezi kuopatikana katika umoja huo,bali kwa njia ya mazungumzo.