Palestina-UN

Palestina yaendelea kushinikizwa kutoka mataifa kadhaa iachane na mpango wa kuomba nafasi UN

Le président palestinien Mahmoud Abbas, lors de son discours télévisé annonce son intention de demander d’adhésion du nouvel Etat de la Palestine à l'ONU, le 16 septembre 2011, à Ramallah.
Le président palestinien Mahmoud Abbas, lors de son discours télévisé annonce son intention de demander d’adhésion du nouvel Etat de la Palestine à l'ONU, le 16 septembre 2011, à Ramallah. REUTERS/Darren Whiteside

Ikiwa imebaki siku moja kupita na kushuhudia nchi ya Palestina ikiwasilisha hoja katika barazala umoja wa mataifa kupatiwa uanachama wa kudumu wa Umoja huo, shinikizo zaidi limeendelea kuongezeka kwa viongozi wake hasa toka kwa serikali ya Marekani na Israel.

Matangazo ya kibiashara

Safari hii magavana wa chama cha Republicans nchini Marekani wamekosoa sera za mashariki ya kati za rais Obama na jinsi anavyoshughulikia mizozo katika maeneo hayo.

Rick Perry Snip On Midle 21.9.2011

Rick Perry Ni gavana wa Jimbo la Texas na hapa anasema kuwa kama isingekuwa sera mbovu za rais Obama kuhusu mashariki ya kati, basi Palestina isingefikia hatua ambayo imefikia leo hii.

 

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al-Malik anasema kuwa anashangazwa na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Marekani katika kuhakikisha nchi yake haiungwi mkono na mataifa mengine na kuongeza kuwa licha ya vikwazo vyote hivyo nchi yake itaendelea na hoja yake siku ya Ijumaa.

Riyad al-Malik Waziri wa Palestina wa mambo ya nje 21.9.2011

 

Siku ya Ijumaa ndio siku ambayo rais wa mamlaka ya Palestina Mahamud Abbas atahutubia baraza la Umoja wa Mataifa na kuwasilisha hoja ya kuomba uanachama huku pia muda mchache ujao akitarajiwa kuwa na mkutano na rais Obama.