Libya

Waasi wa Libya wakiri kupata pigo kubwa katika mji wa Syrte

Msafara wa magari ya wapiganaji wa Libya
Msafara wa magari ya wapiganaji wa Libya Reuters

Wapiganaji wa baraza la serikali ya mpito nchini Libya, wamekiri kuwa wamepata hasara kubwa katika mji wa Sirte kwa kushambuliwa vikali na majehsi ya kanali Muamar Kdhafi tangu walipovamia mji huo wiki iliyopita,na ksuabaisha wanajeshi wake 45 kupoteza maisha yao na kuwajeruhi wengine ambao wamesafirishwa nje ya libya kupta matibabu.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo,wapiganaji hao wansema kuwa wamefaulu kuyataeka maeneo kadhaa ya mji wa Sabha mji ambao unaelezwa kuwa makao makuu ya wanajeshi wanaoumuunga mkono Kadhafi.

Kiongozi wa majeshi ya NATO, Anders Fogh Rasmussen anasema kuwa majeshi hayo yataendelea kushambulia miji hiyo, hadi atakapopatikana Kadhafi.

Wakati hayo yaripotiwa, serikali ya mpito imesema kuwa inatarajia kuunda serikali mpya kwa siku kumi zijazo.