Kenya-ICC

Washukiwa wengine wa mauaji ya baada ya uchaguzi nchini Kenya wasikilizwa na ICC

makamu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta mbele ya korti kuu ya ICC
makamu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta mbele ya korti kuu ya ICC AFP PHOTO/ANP/BAS CZERWINSKI/POOL

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague Uholanzi, wameanza kusikiliza mashtaka yanayowakabili washukiwa wengine watatu wanaotuhumiwa kufadhili na kuchochea machafuko nchini Kenya, ikiwa wana kesi ya kujibu au la, baada ya machafuko hayo ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2007, yaliyosababisha mauji ya zaidi ya watu elfu moja na maelfu kutoroka makwao.

Matangazo ya kibiashara

Watatiu hao ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu aliyepia waziri wa fedha katika serikali ya muungano nchini humo, Uhuru Kenyatta,Mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na aliyekuwa kamishena wa polisi kipindi hicho,Hussein Ali.

Washukiwa hao wanatuhumiwa kupanga mauji na mashambulizi dhidi ya wafuasi wa chama cha ODM, mjini Nakuru na Naivashama katika mkoa wa bonde la ufa nchini humo.

Vikao hivyo vintarajiwa kuendlea hadi mapema mwezi ujao,kundi la washukiwa watatu wa kwanza wakiwa ni wanasiasa William Ruto,na Henry Kosgey pamoja na mtangazaji Joshua Arap Sang wanasubiri hatma yao baadaye mwaka huu ikiwa wana kesi ya kujibu au la.