Libya

Waziri mkuu wa Libya ahidi kuunda serikali katika siku 10 zijazo

Mahmoud Jibril waziri mkuu wa Libya
Mahmoud Jibril waziri mkuu wa Libya REUTERS/Stringer

Ikiwa ni siku moja imepita toka baraza la Umoja wa Mataifa lipige kura na kukubali rasmi kuitambua serikali mpya ya Libya, waziri mkuu wa Libya Mahamud Jibril amesema kuwa anatarajia kuona serikali mpya inaundwa ndani ya siku kumi zijazo.

Matangazo ya kibiashara

Mahamud Jibril 21.9.2011

Jibril ameyasema hayo muda mfupi baada ya kukutana na rais wa Marekani Barack Obama ambapo waziri mkuu huyo ameahidi mabadiliko makubwa nchini mwake kwa kushurikiana na mataifa mengine.

 

Kwa upande wake rais wa marekani Barack Obama amesema kuwa anafahamu chanagmoto nyingi ambazo zitaikabili serikali ya Libya na kuongeza kuwa wapo watu ambao watahoji na kutamani sana kurejea kwa utawala wa zamani na kusisitiza kuwa nchi yake itasimama na serikali mpya katika kuijenga Libya.

Barack Obama 21.9.2011