Palestina-Afrika kusini

Afrika Kusini yaunga mkono ombi la Palestina la kutaka kuwa taifa huru

Reuters

Afrika kusini imesema inaiunga mkono Palestina na mpango wake wa kuomba uanachama wa kudumu ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema kuwa hatua hiyo ya Palestina ni muhimu katika kuleta Amani ya kudumu katika maeneo yenye mizozo.

Zuma ametaka mataifa wanachama wa umoja wa mataifa kuangalia kwa makini ombi la rais wa Palestina, Mahmoud Abbas na kulipitisha.

Marekani imeapa kutumia kura yake ya Turufu kuzuia palestina kutopatiwa uanachama kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zimesema hawatafikia maamuzi yeyote ya kura mpaka pale watakapoona azimia la Palestina.